Na Mwandishi Wetu
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umeuomba uongozi wa Mkoa wa Lindi kuhakikisha unahoji na kusimamia matumizi ya fedha za tele kwa tele zinazolipwa na Mfuko huo kwa halmashauri.
Fedha hizo ambazo zinalipwa na NHIF zinatakiwa kutumika katika ununuzi wa dawa na uboreshaji wa vituo vya kutolea matibabu ili hatimaye kuondokana na mazingira duni ya kutolea huduma.
Ombi hilo lilitolewa juzi na Meneja wa NHIF, Mkoa wa Lindi Fortunata Raymond katika kikao cha Kamati ya Ushauri cha Mkoa ambacho kilijadili mambo mbalimbali ikiwemo taarifa ya utekelezaji ya Mfuko huo ya mkoa.
Akiwasilisha taarifa hiyo, Raymond alisema changamoto kubwa ambayo Mfuko umekuwa ukipambana nayo ni pamoja na fedha hizo kutotumika kama miongozo inavyotaka.
“Sisi kama Mfuko tunaomba sana mtusaidie katika usimamizi wa fedha hizi ikiwemo kuhoji namna zinavyotumika…haiwezekani vituo viendelee kuwa na hali duni huku fedha zinazoweza kuviboresha zikitumiwa katika matumizi yasiyostahili,” aliomba Raymond.
Alisema kuwa endapo fedha hizo zitatumika kama ilivyoelekezwa wananchi watapata huduma za matibabu zinazostahi na katika mazingira mazuri.
Raymond pia alitumia nafasi hiyo, kuhamasisha viongozi hao kutumia fursa inayotolewa na NHIF ya mikopo ya vifaa tiba na ukarabati wa majengo ili kuboresha huduma hususan katika maeneo ya vijijini.
Akijibu baadhi ya hoja, Mkuu wa Mkoa wa Lindi Lodovick Mwananzila aliwataka wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri kuhakikisha fedha hizo zinatumika kwa kufuata mwongozo uliopo.
Alisema hatasita kuchukua hatua kali kwa halmashauri itakayobainika kutumia fedha hizo kinyume na malengo yake.
“Afya ni kila kitu, ili wananchi wetu wazalishe ni lazima wawe na uhakika wa kupata matibabu …na natoa mwito kuwahamasisha wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwa kuwa ndio njia pekee ya kuwasaidia.
Tuesday, September 18, 2012
HALMASHAURI ZITAKAZOTUMIA FEDHA ZA TELE KWA TELE KWA MATUMIZI YASIYOKUSUDIWA KUKIONA-RC LINDI
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Ludovick Mwananzila,akiwautubia washiriki wa mkutano wa kamati ya ushauri ya Mkoa (RCC)ambapo yeye ni mwenyekiti wake,mambo mbalimbali ya maendeleo ya Jamii na kiuchumi yalijadiliwa.Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa mkuu wa Mkoa wa Lindi hivi karibuni.
Meneja mwakilishi wa NHIF ofisi ya Mkoa wa Lindi,Fortunata Raymond,akitoa mada kuhusu utekelezaji wa shughuli za mfuko huo katika Baraza la Ushauri la Mkoa.
Washiriki wa kikao cha baraza la ushauri la Mkoa ambao ni Wakuu wa Wilaya wakifuatilia kwa makini hotuba ya mwenyekiti wa mkutano huo ambaye ni mkuu wa Mkoa wa Lindi Ludovick Mwananzila.
Waheshimiwa wabunge wa Mkoa wa Lindi ni miongoni wa wadau wakubwa kwenye Mkutano wa Baraza la Ushauri wa Mkoa,pichani Mhe. Zainab Kawawa akichangia hoja kwenye mkutano huo. (picha Na. Paul Marenga)
Tuesday, September 11, 2012
NHIF YATOA MSAADA WA VITABU 50 VYA MASWALI NA MAJIBU YA MTINDO BORA WA MAISHA
BI FORTUNATA RAYMOND MENEJA MWAKILISHI WA NHIF MKOA WA LINDI AKIMKABIDHI BI ANNA MARO MSAADA WA VITABU 50 VYA MTINDO BORA WA MAISHA NA MAGONJWA SUGU YASIYOAMBUKIZWA.
BAADA YA MAKABIDHIANO
TASWIRA KIJIJINI NANGOO WILAYANI MASASI
SAA 7 MCHANA BADALA YA KUJIUNGA NA VIKUNDI VYA UZALISHAJI MALI,MCHEZO WA BAO UNACHUKUA MKONDO
Subscribe to:
Comments (Atom)
