Mkuu wa mkoa wa Lindi MH.Ludovick Mwananzila akizungumza kwenye baraza la madiwani wa Wilaya ya Kilwa kuhusu uhamasishaji wa wananchi kujitokeza kwenye zoezi la kuhesabiwa litakalofanyika kitaifa nchi nzima,madiwani hao wanaendelea na kikao cha kazi wilayani humo.
Madiwani wa Wilaya ya Kilwa wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Mh.Ludovick Mwananzila hayupo pichani wakati akishiriki kwenye kikao cha baraza hilo.
Mkuu wa Mkoa wa lindi Mh.Ludovick Mwananzila ametoa rai hiyo mbele ya kikao cha baraza la madiwani wa Wilaya ya Kilwa,kuwahamasiha wananchi wengi kujitokeza na kutoa taarifa sahihi kwa maafisa watakao kuwa na jukumu,ili kufanya zoezi kuwa na tija kwa taifa siku ya tarehe 26/08/2012.
mkutano huo wa kitendaji wa baraza la madiwani unaendelea katika ukumbi wa Jumba la Maendeleo chini ya uenyekiti wa Mh.Farida Kikoleka-makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya kilwa

No comments:
Post a Comment