Thursday, July 5, 2012

MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA WAADHIMISHA MIAKA KUMI TANGU KUANZISHWA

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umeadhimisha miaka kumi kwa kutoa tuzo kwa mashujaa mbalimbali waliochangia katika mafanikio yake tangu kuanzishwa. Mashujaa hao ni pamoja na viongozi wakuu wa serikali wastaafu, mawaziri wastaafu, viongozi wa vyama vya wafanyakazi, watumishi wa serikali wastaafu na waandishi wa habari.

Akikabidhi tuzo hizo Mhe. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Peter Pinda alisisitiza umuhimu wa Halmashauri kusimamia vema fedha zinazotolewa kama malipo ya tele kwa tele na kumwagiza Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali, kufanya ukaguzi wa matumizi ya fedha hizo katika halmashauri.

Aidha aliugiza uongozi wa NHIF kuhakikisha kuwa unayafanyia kazi mapema malalamiko ya wanachama hususan ya ucheleweshaji wa vitambulisho na utoaji wa vibali vya matibabu. Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Mhe. Benjamin William Mkapa ni miongoni mwa mashujaa wa NHIF waliokabuidhiwa tuzo maalumu katika sherehe hizo.

No comments:

Post a Comment